Pangani FM

Polisi Pangani yaitaka Jamii kushiriki kikamilifu kutoa ushahidi.

3 December 2020, 12:58 pm

Jeshi la Polisi wilayani Pangani mkoani Tanga, limeitaka jamii kushiriki kikamilifu kutoa ushahidi pale ambapo mwananchi atakuwa ameshuhudia tukio fulani la ukatili au uhalifu wowote ili kesi ziweze kufikia mwisho.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa upelelezi wilaya ya Pangani ASP ELIJA MATIKU alipotembelewa na kituo hiki ambapo amesema kuwa wananchi wanapaswa kutoa ushahidi na kueleza ukweli wa yale waliyoyaona ili kusaidia Mahakama kufikia maamuzi kwa wakati.

Aidha ASP MATIKU amebaisha kuwa kesi nyingi za ukatili zinatokea kati ya ndugu na ndugu na kwamba zinapotezwa ushahidi kutokana na tabia ya baadhi ya wananchi kuyamaliza masuala hayo kwa taratibu ambazo sio sahihi na rasmi.

Hayo yamekuja kufuatia kesi nyingi za ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto  kutofikia mwisho kutokana na kukosekana kwa ushahidi Mahakamani. Tanzania na Mataifa mengi Ulimwenguni yapo katika Siku 16 za kupinga ukatili ambazo kwa mwaka 2020 kauli mbiu inasema TUPINGE UKATILI WA KIJINSIA MABADILIKO YANAANZA NA MIMI.