Pangani FM

Shilole atoa wito huu kwa wazazi Mitandaoni.

6 March 2023, 10:03 pm

Msanii Shilole akizungumza na wananchi Pangani.

Msanii wa muziki na mjasiriamali maarufu Tanzania Bi. Zuwena Mohamed maarufu kama ‘Shilole’ ametoa wito kwa  wanawake kuwalinda  watoto wao dhidi ya vitendo vya ukatili vinavyoweza kutokana na  matumizi ya mitandao ya kijamii.

Shilole alikuwa moja ya wageni walopata afas ya kuzungumza katika Jukwaa la maadhimisho ya siku ya wanawake yaliyofanyika wilyani Pangani Jumapili Machi 5, 2023 na alitumia jukwaa hilo kutoa wito huo kwa wazazi.