Pangani FM

Wakazi wa Pangani watakiwa kuchukua tahadhari kabla ya msimu wa mvua za El nino

21 September 2023, 12:46 pm

Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi Zainab Abdallh Issa

“nawaomba wananchi wanaoishi maeneo ambayo yanapitiwa na mafuriko kuhama kabla mvua hazijaanza”

Na Maajabu Ally

Wananchi wanaoishi katika maeneo ya bondeni Wilayani Pangani Mkoani TANGA wametakiwa kuchukua tahadhari kufuatia taarifa za uwepo wa mvua za El nino

Tahadhari hiyo imetolewa na mkuu wa Wilaya hiyo Bi Zainabu Abdallah Issa wakati akizungumza na kituo na Pangani Fm katika kipindi cha “Asubuhi ya Leo”

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani

Bi ZAINABU pia amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuweka akiba ya chakula ili kujiepusha na athari zinazoweza kujitokeza.