Pangani FM

Ushiriki wa wanawake katika utunzaji na ulinzi wa mazingira ya bahari

12 May 2026, 12:41

Mwanamke akiwa katika shughuli ya uchambuaji wa zao la Mwani linalotumika katika ulinzi wa mazingira ya bahari

Na Rajabu Mrope

Karibu maeneo mengi ambayo yana Bahari nchini Tanzania,kumeundwa kamati za BMU kirefu chake ni neo la Kiingereza,Beach Management Unit,nak ama ati hizi zikihusika na ulinzi wa Bahari na mazingira yake katika kudhibiti uharibifu wa mazingira kama vile kutumia zana zisizoruhusiwa au zinazoharibu mazalia ya Samaki.

Jumla ya vijiji 33 wilayani Pangani vina kamati za BMU 13 wakati kila kamati ikiwa na wajumbe 30, zaidi ya nusu ni wanawake ambao wanashiriki katika kujadili,mipango na sera za utunzaji wa mazingira hususani Bahari.

Katika vijiji 33 vilivyopo wilayani Pangani 39%  ya vijiji vina kamati na BMU na ndio vijiji ambavyo vimepitiwa na Bahari.