Pangani FM
Pangani FM
26 May 2026, 10:41

Ujenzi wa daraja la Mto pangani lenye urefu wa mita 525, kwa sasa ndilo tumaini jipya la Wananchi katika kutafuta suluhusho ya kudumu la mawasiliano wilayani Pangani.
Kabla ya daraja hili kuanza kujengwa wanawake walikuwa wakijifungua katika kijiji cha Bweni eneo la kivukoni hasa nyakati za usiku kutokana na kukosekana kwa kivuko ambacho hufanya kazi mwisho saa nne usiku, pamoja na hayo kivuko hicho kimekuwa kikisitisha huduma zake mara kwa mara kutokana na hitilafu.
Kutokana na hali hiyo serikali ilichukua hatua kwa kuanza ujenzi wa daraja unaokwenda sambamba na barabara unganishi ambapo shilingi Bilion 124.9 zimetengwa kwaajili ya kufanikisha ujenzi wa daraja hilo, linalotarajiwa kukamilika mwaka 2027.
Ungana na Majabu Madiwa kupata simulizi ya namna daraja hilo lilivyoleta safari salama kwa mama wajawazito.