Pangani FM

Serikali kuwashika mkono watu wenye ulemavu

27 July 2026, 14:07

Baadhi ya washiriki katika mafunzo maalumu yaliyowakutanisha viongozi wa vikundi vya walemavu katika wilaya ya Pangani yanayotolewa na shirika la UZIKWASA. Picha na Cosmas Clement.

Nataka kuwahakikishia serikali imeanzisha mfumo maalumu kwa ajili ya walemavu utakaotumika kutambua idadi ya walemavu ili kufikia utatuzi wa mahitaji yao”, Bwana Tadei Kamisa.

Na Cosmas Clement

Shirika la UZIKWASA  limekutana na wawakilishi wa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali wilayani Pangani kwa ajili ya mafunzo ya kukabiliana na changamoto  zinazowakabili ikiwemo ukatili na mabadiliko ya tabia nchi kupitia nguvu, na nafasi walizonazo.

Akizungumza kuhusu mafunzo Mwezeshaji kutoka shirika la UZIKWASA Bwana Joseph Peniel Amesema mafunzo hayo ni mwendeezo wa mafunzo yanayotolewa na shirika hilo katika kuwahudumia wananchi wa ndani na nje wilaya ya Pangani.

Sauti ya bwana Joseph Peniel mwezeshaji kutoka UZIKWASA
Baadhi ya viongozi wa vikundi vya walemavu wakiwa na baadhi ya maafisa ustawi na maendeleo ya jamii wa kata wilayani Pangani.

Akifungua mafunzo hayo Afisa ustawi wa jamii wilaya ya Pangani Bwana Tadei Kamisa ameipongeza shirika hilo kwa kuanzisha mafunzo kwa kundi hilo ambayo yatasaidia katika kuwawezesha kunufaika na fursa mbalimbali zitolewazo na serikali.

Sauti ya bwana Tadei Kamisa afisa ustawi wa jamii wilaya ya Pangani

Bwana Kamisa amesema kwa sasa serikali inaendelea kutekeleza mikakati endelevu na kwamba serikali ina lenga kuwakomboa walemavu.

Sauti ya bwana Tadei Kamisa afisa ustawi wa jamii wilaya ya Pangani

Mafunzo yanayotolewa na shirika la UZIKWASA kwa watu wenye ulemavu katika wilaya ya Pangani yameanza leo jumatatu yanatarajiwa kufikia tamati Jumanne July 28 2026.