Pangani FM

Vitendea kazi kwa maafisa ugani,chachu ya mageuzi ya kilimo wilayani Pangani

17 June 2026, 16:56

Bwana Silevester Japhet Manga mkulima wa mpunga katika bonde la kitivo wilayani Pangani: Picha na Cosmas Clement

“Kwahiyo mara ya kwanza kukodi pikipiki ilikuwa ni changamoto kwahiyo mkulima akipata changamoto ilikuwa ni ngumu kufikia, hivyo wakulima walikuwa wanalima kwa namna wanavyoweza wao, lakini uwepo wa pikipiki hizi na vishikwambi imesaidia kuwafikia wakulima katika mashamba na kuchangia ongezeko kubwa la uzalishaji”. Amesema Afisa Ugani Masaika Bwana Patrick Mavunga.

Na Cosmas Clement

Sekta ya Kilimo imeendelea kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania ikikadiriwa kutoa ajira kwa takribani ya asilimia 65.6  ya nguvu kazi ya Taifa na kuchangia asilimia 24.6 ya pato la taifa kwa kipindi cha mwezi januari hadi September 2025.

Licha ya mchango wake katika nchi, sekta hii imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo huduma duni za ugani.

Hata hivyo Serikali ya awamu ya sita kwa kutambua changamoto hii imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo kugawa vitendea kazi kwa maafisa ugani ili kuongeza chachu katika mageuzi katika sekta ya kilimo.

Miongoni mwa mikakati hiyo ni ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa ugani. Makala hii inasimulia shuhuda za wakulima wanavyonufaika na mpango huo.

Sikiliza hapa makala iliyoandaliwa na Cosmas Clement.