Pangani FM
Pangani FM
3 April 2026, 15:05

Na Hamisi Makungu
Mpango wa Serikali unaosimamiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), umefanikiwa kuwawezesha wavuvi wa Mkoa wa Tanga kunufaika kupitia Uchumi wa buluu.
Mpango huo ambao unatekelezwa kwa awamu umepelekea kuongeza tija, ajira na kukuza uchumi kupitia uvuvi endelevu.
Wakati Serikali ikiendelea kuweka mazingira bora ya kuongeza ajira, kuinua kipato cha wavuvi na kufikia lengo la kuongeza mchango wa sekta ya uvuvi katika Pato la Taifa hadi asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.
Zaidi ya asilimia 45 ya mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani yanatokana na shughuli za uvuvi, hivyo kupitia Makala hii iliyoandaliwa na Hamisi Makungu baadhi ya wanufaika wa mpango huo Pangani wamefikiwa ili kuona tija iliyopatikana hadi sasa.