Pangani FM

Nishati ya solar yaweka mwanga salama wakati wa kujifungu

30 August 2025, 20:04

Jengo la zahanati ya Mtaa wa Marungu katika halmashauri ya jiji la Tanga

Na Maajabu Madiwa

Nishati ya solar katika zahanati ya mtaa wa marungu iliyopo halmashauri ya jiji la Tanga inatajwa kuleta mwanga salama kwa wanawake wakati wa kujifungua .

Hatua hii inatokana na mahusiano mazuri yaliyowekwa baina ya serikali na wadau yaliyopelekea wanawake kuondokana na changamoto ya kujifungua kwa tochi hasa pale umeme unapokatika nyakati za usiku.

Kabla ya hatua hii ya serikali wanawake wanapojifungua usiku hasa pale umeme unapokatika wamekuwa katika hatari ya kujifungua kwa kumulikiwa kwa tochi jambo ambalo linawaweka hatarini wanawake hao,watoto wanapozaliwa na hata watoa huduma.