Pangani FM
Pangani FM
4 June 2026, 11:43

Na Rajab Mrope
Serikali ya Tanzania inatekeleza Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mkopo wa Dola za Marekani milioni 500 sawa na takribani Trilioni 1.2 za Kitanzania inatekeleza uboreshwaji wa elimu ambapo mingoni mwa Vipaumbele vya Matumizi ya Fedha ni Ujenzi wa Shule na Mabweni na na kuboresha miundombinu mingine ya elimu.
Mpango wa mabweni kwa wasichana umeonekana kuzaa matunda kufuatia takwimu za Utafiti wa Afya na Demografia Tanzania (THDS-MIS) za mwaka 2022 zinaonyesha kiwango cha mimba za utotoni kimepungua.
Kupitia makala hii utasikia simulizi ya kuvutia, juu ya namna ufaulu wa wananfunzi wa kike wilayani Pangani unapaa kutokana na uwepo wa Mabweni.