Pangani FM

Simba wavamia na kuua mifugo Pangani.

10 May 2023, 12:12 pm

Wananchi wilayani Pangani Mkoani Tanga hususan wanaokaa ng’ambo ya mto Pangani kuanzia kijiji cha Bweni wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya wanyama aina ya Simba waliovamia baadhi ya vijiji.

Kuanzia mwisho wa mwezi Aprili mwaka 2023 kumekuwa na matukio ya kuonekana kwa wanyama aina ya samba katika vijiji vya Langoni,Mwera, Kikokwe, Mtango, na Mzambarauni ambao tayari wameua Ng’ombe wanne, Mbuzi 8, Kondoo mmoja na Mbwa mmoja. Leo Pagani FM imefanya mahojiano na Afisa Mahusiano (Ujirani mwema) kutoka hifadhi ya Taifa ya Saadan bwana Romanus Galus Mponda ambaye amethibitisha uwepo wa Simba hao na tayari Askari wa wanyamapori wako katika maeneo mbalimbali ya vijiji vya Pangani kufuatilia walipo Simba hao ili kufanya taratibu za kuwaondoa kwenye makazi ya watu.

Afisa Mahusiano (Ujirani mwema) kutoka hifadhi ya Taifa ya Saadan bwana Romanus Galus Mponda katika Studio ya Pangani FM.

“Ni kweli kuna simba wawili ambao wanasumbua jamii,jitihada zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi na viongozi kuwafuattlia, lakini wananchi watoe taarfa wanapowaona ili kuweza kupata msaada wa haraka Zaidi ila jitihada zinaendelea kuwafanya wananchi wawe na Amani”

Amesema Bwana Mponda.

Sauti ya Afisa Mahusiano (Ujirani mwema) kutoka hifadhi ya Taifa ya Saadan bwana Romanus Galus Mponda katika Studio ya Pangani FM.

Bwana Mponda amesema kuwa mwnenendo wa Simba na wanyama wengine kuvamia maeneo ya watu umechangiwa pia na uharibifu wa mazingira pamoja na shughuli za binadamu katika maeneo ya karibu na hifadhi.

“Kuna changamoto ya binadamu kuwa karibu na mipaka ya hifadhi, wakati Fulani wafugaji pia wanafuga karibu na mipaka ya hifadhi hali inayopelekea changamoto kama hizi”

Amesema Bwana Mponda

Sauti ya Afisa Mahusiano (Ujirani mwema) kutoka hifadhi ya Taifa ya Saadan bwana Romanus Galus Mponda katika Studio ya Pangani FM.

Pamoja na jithada hizo bwana Mponda amesema kuwa wameendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuchukua tahadhari pamoja na kufahamu hatua za kuchukua katka matukio kama hayo Ikiwemo mfumo wa kupata fidia kutokana na uvamizi wa wanyamapori hivyo amestitiza wananchi kutoa taarifa kwa viongozi wa eneo husika.

Hifadhi ya Taifa ya Saadani imepakana moja kwa moja na vijiji vya wilaya za chalinze, Bagamoyo, Handeni na Pangani ambapo kwa wilaya ya Pangani inapakana na vijiji vya Mkalamo,Sange,Kwakibuyu, Mikocheni,Mkwaja, Buyuni na Mburizaga