Pangani FM

MIA za Rais Samia Pangani-Umeme

29 June 2021, 12:26 pm

Shirika la Umeme TANESCO Wilayani Pangani Mkoani Tanga layaelezea Mafanikio yake katika kuwahudumia wananchi ndani ya Siku 100 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na Pangani FM leo Meneja wa TANESCO Wilayani humo Bwana. PETER DISMAS MWAIMU, amesema katika Siku 100 za Rais Samia Madarakani, wamefanikiwa kuwasogezea wananchi huduma ya Umeme hasa katika maeneo ambayo hayakuwa na huduma hiyo.

Aidha Bwana. Peter amesema TANESCO ina matarajio makubwa na Rais Samia, kutokana na kasi aliyoionesha kwa Siku 100 katika Uongozi wake.

sikiliza hapa

Serikali iko katika utekelezaji wa mradi wa Kusambaza Umeme vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili ambapo kwa wilaya ya Pangani vijiji vya Mzambarauni, Buyuni na Langoni ndivyo vimesalia bila Umeme.