Pangani FM

Nguvu ya mafunzo ya mguso kuboresha vyombo vya habari

14 March 2023, 1:13 pm

Mwezeshaji kutoka Shirika la UZIKWASA Bi. Salvata Kalanga akizungumza katika moja ya mijadala inayoendelea kwenye mafunzo hayo. Picha na Erick Mallya

Kwa miaka mingi Shirika la UZIKWASA limekuwa likitoa mafunzo ya ‘mguso’ ambayo yamekuwa yakiwawezesha watu binafsi kutafakari nafasi zao katika kuchochea mabadiliko chanya pamoja na mabadiliko ya kitaasisi na Jamii kwa ujumla.

Na Erick Mallya

Mwezeshaji kutoka Shirika la UZIKWASA Bi. Maimuna Msangi akiendesha moja ya mijadala ya mafunzo ya mguso. Picha na Erick Mallya

Shirika la UZIKWASA lililopo wilayani Pangani Mkoani Tanga kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeanza rasmi mafunzo maalumu ya siku 4 yanayowakutanisha viongozi waandamizi wa vyombo vya Habari vya Tanzania bara na visiwani

Mafunzo hayo yanayoendelea katika moja ya Kumbi za mikutano za Royal Village zilizopo jijini Dodoma yenye lengo la ‘kuwezeshana kwa pamoja kama viongozi wa vyombo vya Habari juu ya kutafakari na kuzingatia masuala ya jinsia kwa kutumia mbinu wezeshi (Mguso) yameanza Jumatatu Machi 13 na yanatarajiwa kukamilika Machi 16 kwa awamu ya kwanza inayohusisha viongozi wa vituo vya Redio.

Mkurugenzi wa Irangi FM Bi. Saumu Sakala ameshukuru uwepo wa mafunzo hayo kwani yamempa nafasi ya kufikiria upya umuhimu wa kujitathmini kama kiongozi wa chombo cha Habari.

Mkurugenzi wa Irangi FM Bi Saumu Sakala
Sauti ya Mkurugenzi wa Kitu cha Irangi FM Bi. Saumu Sakala.

“Nilikuwa nawafikia kwa kusema kwa juu juu lakini sio kwa uzito, kwa kupitia mafunzo haya imenifanya nione kuna kitu ambacho kilikuwa ni muhimu sana kama jukumu lakini nilikuwa nikipuuzia ni muhimu wote kufanya self reflection”

Amesema Bi Saumu Sakala.

Nao washiriki wengine wa mafuzo hayo kutoka Kituo cha tripple A kilichopo jijini Arusha pamoja na Kilosa FM wameeleza namna mafunzo hayo yalivyowaonyesha baadhi ya maeneo ya kuyafanyia kazi kwenye vituo vyao ili kuboresha uzingatiaji wa masuala ya Jinsia kiutendaji na hata katika maudhui.

Sauti ya Washiriki wengine wa Mafunzo hayo.

Kwa miaka mingi Shirika la UZIKWASA limekuwa likitoa mafunzo ya ‘mguso’ ambayo yamekuwa yakiwawezesha watu binafsi kutafakari nafasi zao katika kuchochea mabadiliko chanya pamoja na mabadiliko ya kitaasisi na Jamii kwa ujumla.

Wanufaika wa mafunzo hayo wamekuwa vongozi wa dini, viongozi wa taasisi, waandishi wa habari, vongozi wa kisiasa na wale wanaosimamia masuala ya Jinsia na Mazingira.

Faida za mafunzo hayo zimetambulika katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa.

Wawezeshaji kutoka Shirka la UZIKWASA Kushoto Bi. Salvata Kalanga pamoja na Bw. Edward Saguti wakonyesha kwa vitendo umuhimu wa Viongozi kusikiliza. Picha na Erick Mallya

Mwezeshaji kutoka shirika la UZIKWASA Bi. Salvata Kalanga ameeleza kuwa mategemeo ya shirika la UZIKWASA kutokana na mafunzo hayo ni pamoja na kufanya masuala ya jinsia kujadiliwa katika vyombo vya Habari kwa ukubwa.

Mwezeshaji kutoka Shirika la UZIKWASA Bi. Salvata Kalanga. Picha na Erick Mallya
Sauti ya mwezeshaji kutoka Shirika la UZIKWASA Bi. Salvata Kalanga.