Pangani FM

Jamii Tanga yaaswa kuzingatia lishe, kujenga afya bora

29 October 2023, 4:03 pm

Afisa lishe (W) ya pangani Daud Mwakamnge akielezea matumizi ya lishe bora

“kuanzia miaka 10 hadi 19 ni umri wenye tabia za ulaji wa vyakula vyenye mafuta,sukari na chumvi na kutokula mboga mboga na matunda”

Halmashauri ya Wilaya ya Pangani mkoani Tanga imeadhimisha siku ya lishe katika ofisi ya kata ya Pangani Magharibi iliyopo Pangani mjini huku jamii ikiaswa kuzingatia lishe bora ili kujenga afya zilizobora.

Akiongea wakati wa maadhimisho hayo Afisa lishe Wilaya ya Pangani DAUDI MWAKABANJE amesisitiza lishe bora kwa vijana balehe kwakuwa kundi hilo linaongoza kwa kula vyakula vyenye mafuta,sukari na chumvi na kutokula mboga mboga na matunda.

Sauti ya Afisa Lishe (W) ya Pangani Daudi Mwakabanje
Baadhi ya wadau walioudhuria maadhimisho ya siku ya lishe katika wilaya ya Pangani

Afisa lishe huyo amesema ulimwengu  uko katika vuguguvu la kutambua vijana kama kundi maalum kwahiyo siyo vizuri kwa kundi hilo kukabiliwa na upungufu wa lishe bora.

Sauti ya Afisa Lishe (W) ya Pangani Daudi Mwakabanje

Maadhimisho hayo pia yamewashirikisha wadau wa maswala ya lishe kwa vijana balehe likiwemo shirika lisilo la kiserikali la Afriwag ambapo mwakilishi kutoka shirika hilo BI FATMA HAMZA amewasihi wazazi kuzingatia suala la lishe bora kwa watoto wao

Sauti ya Mwakirishi kutoka shrike la  Afriwag BI FATMA HAMZA

Wilaya ya Pangani ina Udumavu kwa asilimia 1,uzito uliopitiliza asilimia 0.2,ukondefu asilimia 0.8 na upungufu wa damu kwa mama wajawazito ni asilimia 4.7

Maadhimisho ya siku ya kitaifa ya lishe kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo ‘’LISHE BORA KWA VIJANA BALEHE ,CHAHU YA MAFANIKO YAO