Pangani FM
Pangani FM
15 May 2026, 11:57

Na Rajabu Mrope
Mwalo wa Kipumbwi, ndani ya Wilaya ya Pangani ndipo kitovu cha uvuvi ambapo boti zaidi ya 400 na wavuvi zaidi ya 6000 kutoka ndani nan je ya wilaya ya Pangani wanajishghulisha na shuhguli hii.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mchanganuo wa Idadi ya Ajira kwa Shughuli za Kiuchumi Mwaka
2023/24 zimechangia ajira za muda mrefu 122,380 za muda mfupi 65,823 na imechangia pato la taifa kwa 4.7 %.
Kutokana na hilo Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), imekabidhi rasmi eneo la ujenzi wa Soko la Samaki la Kimataifa Kipumbwi, wilayani Pangani mkoani Tanga, mradi unaotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.3.
Mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi WCEC Limited kama sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha sekta ya uvuvi na kuongeza ushindani wa bidhaa za uvuvi katika soko la ndani na kimataifa.
Rajabu Mrope anatupasha undani wa taarifa hii. Hapa