Pangani FM

Waliokatiza masomo wilayani Pangani, wahimizwa kurudi shuleni kupitia mfumo rasmi wa elimu

25 May 2026, 23:06

Picha ikionyesha baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Funguni wilayani Pangani. Picha na Mwandishi wetu

Ingawa utaratibu wa kuwarejesha wanafunzi waliokatisha masomo ulianza kutekelezwa kabla, maboresho ya sera na mwongozo yameufanya utekelezaji kuwa wazi zaidi.

Na Saa Zumo

Serikali imeandaa Mwongozo wa Kuwarejesha Shuleni Wanafunzi Waliokatiza Masomo katika Elimu ya Msingi na Sekondari kwa Sababu Mbalimbali ili waweze kukamilisha mzunguko wa masomo yao katika mfumo rasmi elimu.

Sasa wanafunzi wanaorejea kupitia mfumo rasmi wa elimu husoma darasa la kawaida pamoja na wenzao, huvaa sare za shule na kushiriki shughuli zote za shule kama wanafunzi wengine.

Hata hivyo, licha ya fursa hiyo kuwepo, katika Wilaya ya Pangani ni mwanafunzi mmoja pekee wa kike aliyekatiza masomo yake ya sekondari mwaka 2025 kurejea tena shuleni kupitia mfumo huu rasmi wa elimu. Huku Afisa elimu sekondari akihimiza wazazi na walezi kuchangamkia fursa hiyo.

Bonyeza hapa kusikiliza makala hii kama ilivyoandaliwa na Saa Zumo