Pangani FM

CAN Tanzania wawezesha jamii wilayani Pangani dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi

1 May 2026, 13:06

Bwana Mkombozi Joannes kutoka CAN Tanzania akiwa studio za Pangani FM.

Shirika la Climate Action Network Tanzania limekuwa likiendesha mradi wa Alligning III ambao unawalenga wakulima, wafugaji na wavuvi katika kuwa na taarifa sahihi za mwenendo wa hali ya hewa kwa msimu na kwa kipindi husika.

Pia kupitia mradi huo unawawezesha wakulima wafufaji na wavuvi kuwa na uwezo wa kuchukua hatua katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabia nchi.

Kutokana na hayo Pangani FM imezungumza na Bwana Mkombozi Joannes kutoka shirika la CAN Tanzania na bwana Gabriel kutoka idara ya kilimo, mifugo na uvuvi wilaya ya Pangani kujua namna gani mradi huo umesaidia.