Chai FM
Chai FM
22 October 2026, 8:49 pm

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Hanniu alimkabidhi kadi ya bima ya afya mmoja ya wananchi [picha na Noah Kibona]
wakazi wa Rungwe wananufaika na Bima ya afya kwa kuwapunguzia gharama za matibabu
RUNGWE MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Vingozi wa serikali za mitaa na vijiji wametakiwa kuendelea kuwahimiza wananchi katika maeneo yao kuhakikisha kila mwananchi ana kuwa na Bima ya afya kwa wote iliyo boreshwa ili kujenga jamii yenye afya bora
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh, Jaffar Hanniu wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Bima ya afya kwa wote awamu ya pili iliyofanyka kwenye uwanja wa michezo wa shule ya msingi Bulyaga iliyopo kata ya bulyanga wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya
Mkuu huyo wa wilaya amesema serikali hapendi kuona wananchi anakosa fursa ya kupata taarifa muhimu kuhusu Bima ya afya kwa wote hivyo taasisi zizizo za kiserikali ,viongozi wadini kwakushirikiana na serikali ni vyema kuendelea kuwamasisha wananchi juu ya mpango huo
Sauti ya mkuu wa wilaya 1
Hata hiyo Hanniu amesema halmashauri ya wilaya ya Rungwe kupitia idara ya afya kuhakisha utekelezaji wa mpango huu wa bima ya afya kwa wote unaingizwa katika mipango ya halimashauri na kusimamiwa vizuri na wananchi wanahudumiwa bila ubaguzi
Sauti ya mkuu wailaya 2
Ester Haule ni afisa wanachama mkuu mfuko wa taifa wa Bima ya afya [NHIF] amesema katika wilaya ya Rungwe kwa awamu ya pili imelenga kuwasajili zaidi ya kaya 2000 zenye wanufaika3597 na mesema ili kufika malengo amesisitiza kuwepo kwa ushirikiano kwa ofisi ya mkuu wailaya,wizara ya afya,pamoja na wadau wengine

Baadhi ya wananchi walioshiriki uzinduzi wa awamu ya pili ya Bima ya afya kwa wote[picha na Noaha Kibona]
Sauti ya afisa wanachama mkuu wamfuko wa Taifa wa Bima ya afya[NHIF]
Naye mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Rungwe Dr,Diocres Ngaiza ameishukuru serikali kwa kuazisha huma hii ya Bima ya afya kwa wote kwani kutasaidia familia mbalimbali kuondonana na kushindwa kumudu gharama za matibabu
Sauti ya mganga mkuu wilaya ya Rungwe
Kwa upande wao wananchi walionufaika na huduma ya Bima ya afya kwa wote amesema apo awali kabla ya huduma hii walikuwa wakitumia madawa ya kienyeji baada ya kushindwa kumudu gharama ya matibabu
Sauti za wanufaika na Bima ya afya
Wananchi wamemshukuru Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hasani kwa kuleta mpango huo wa bima ya afya kwa wote kwani umeondoa maumivu walikuwa wakiyapata kabla.