Chai FM

Hatma ya watoto wa kike waliopata ujauzito katika umri mdogo

12 September 2023, 1:37 pm

Mimba za utotoni ni miongoni mwa sababu zinazosababisha wasichana wengi kutotimiza ndoto zao huku takwimu zikionesha asilimia 40 ya wasichana huacha masomo kutokana na mimba, hii ni kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2016 wa Human Rights Watch.

Frida Mwaipopo alikuwa na ndoto za kuwa daktari siku moja, lakini sasa ndoto zake zimeishia kulea mtoto baada ya kupata ujauzito akiwa kidato cha pili kwenye shule ya sekondari ya Mwaya wilaya ya Kyela mkoani Mbeya nchini Tanzania.

Chai FM imetembelea katika kijiji cha Lugombo kilichopo katika kata ya Mwaya wilayani Kyela umbali wa kilomita 11 kutokea makao makuu ya wilaya.