Chai FM

Ukosefu wa pembejeo pamoja na vikundi tazizo wakulima wa Parachichi

15 April 2022, 11:34 am

RUNGWE-MBEYA

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Dr.VICENT  ANNEY amefanya ziara ya kuwatembelea wakulima wa mapachichi kwa lengo la kujua changamoto zinazowakabili katika zao hilo.

Wakulima zao la palachichi wa kijiji cha Ibungila kata ya Malindo wameeleza changamoto zinazowakabili katika zao hilo ikiwa ni ukosefu wa pembejeo pamoja na kukosekana kwa vikundi vya pamoja.

 

Aidha CHRISTOPHER MWENGA ambaye ni mkulima pia ni mjumbe wa AMCOS ya UWAMARU amesema kuwa changamoto kubwa kwa kipindi hiki ni bei ya soko hilo kwani hapo awali waliuza kwa shilingi 1780 kwa kilo na sasa wanauza kwa shilingi 1450 hali iliyochangia kushuka kwa kipito kwa wakulima.

Hata hivyo GETRUDA SAIDI na JESIA KATENDE wanununzi wa zao hilo la parachichi wameeleza changamoto wanazokumbana nazo ikiwa ni kutopanga mjadala wa bei elekezi kabla ya zao hilo kukomaa pamoja na  ubovu miundombinu ya barabara kwani wanashindwa kusafirisha mazao hayo kwa wingi.