Chai FM

Watoto elfu 34 kupatiwa chanjo ya polio halmashauri ya Busokelo.

20 September 2023, 6:18 pm

Mtangazaji wa kipindi cha Chai Yetu leo jioni Lennox Mwamakula akizungumza na mratibu wa chanjo halmashauri ya Busokelo Barick Mhagama kwa njia ya simu( Picha na Sabina Martin)

watoto wenye mahitaji maalum pia wanahaki ya kupata hii chanjo ya polio hivyo msiwafungie ndani wapeni nafasi ya kupata chanjo.

Na Sabina Martin – Rungwe
Wazazi na walezi katika halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa kutowafungia watoto wenye mahitaji maalum na kuwaruhusu wapate chanjo ya polio kwa maslahi mapana ya afya yake.
Akizungumza na Chai FM kwa njia ya simu mratibu wa chanjo halmashuauri ya Busokelo Bw. Barick Mhagama amesema kuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wazazi na walezi wa watoto wenye mahitaji maalum kuwafungia ndani watoto hao hivyo kukosa haki ya kupata chanjo hiyo ya Polio.

Sauti ya mratibu wa chanjo mhagama kuhusu watoto wenye ulemavu

Aidha Bw. Barick Mhagama Amesema kuwa kwa halmashauri ya Busokelo chanjo hiyo itatolewa katika vituo 25 vya kutolea huduma za afya, kwenye nyumba za Ibada pamoja na kupitia nyumba kwa nyumba huku walengwa wakiwa ni watoto wote wenye umri wa mwaka 0 hadi miaka nane.

Kwa mujibu wa Mhagama amesema halmashauri ya Busokelo inatarajia kuchanja watoto elfu 34 katika maeneo tofauti yaliyo ainishwa ya vituo vya afya, nyumba kwa nyumba, nyumba za ibada na hata katika maeneo ya sokoni na gulioni.

Sauti ya mratibu wa chanjo kuhusu vituo vya kutolea huduma

Chanjo ya polio inaanza kutolewa kesho alhamis ya tarehe 21 mwezi septemba hadi septemba 24 katika maeneo tofauti mikoa ya Mbeya, Rukwa, songwe, pamoja na kagera.