Chai FM

Serikali kutenga fedha kwajili ya kuboresha miundombinu ya maji Rungwe

28 November 2021, 8:42 am

RUNGWE-MBEYA

Mbunge wa jimbo la Rungwe  ANTON  MWANTONA amesema tatizo la maji linalo wakabili wanachi wa jimbo la Rungwe linaenda kumalizika baada ya serikali kutenga fedha kwajili ya kuboresha miundombinu ya maji

kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungunza na na wananchi wa kata ya Bulyaga wilayani Rungwe Mkoani Mbeya alipo fanya ziara ya kusikiliza kero mbalimbali zinazo wakabili wanachi wa jimbo hilo.

Akisoma taarifa fupi mbele ya Mbunge huyo diwani wa kata hiyo Mh,FURAHA  MWAMBUNGU  ameeleza changamoto ya barabara,daraja la mto Kyala pamoja na jengo la utawala la shule ya sekondari Bulyaga na kumuomba mbunge aweze kuwatatulia

Mwambungu ameungeza kuwa pamoja na jitihada za serikali za uboreshaji wa barabara ya kutoka Tandale kulekea darajani amemuomba mbunge kuwajengea daraja hilo kwani kimekuwa ni kilio cha muda mrefu kwa wakazi wa kata ya Bulyaga

Kwa pande wao wananchi wa kata ya Bulyaga wamemuomba mbunge kuunda kamati ndogo ili kutatua changamoto inayo kwaqmisha maji yasipatikane kwa baadhi ya maeneo katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe

Akijimbu kero hizo mbunge huyo amewaomba wananchi hao kuwa wavumilivu kwakipindi kifupi kwani tayari mkadarasi yupo kazini na mabomba yametandazwa kilometa tatu kutoka  chanzo cha maji