Chai FM

Wananchi Rungwe mjitokeze kuupokea Mwenge

10 September 2022, 7:43 am

RUNGWE-MBEYA.

NA:JUDITH MWAKIBIBI
Wananchi wilayani RUNGWE MKOANI MBEYA wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kuupokea mwenge wa uhuru utakaofika 10sept 2022 ilikuweza kuzindua miradi mbalimbali katika halmashauri.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Rungwe Dk Vicent Anney alipokuwa ametembelea studio za redio Chai ambapo amesema kuwa mwenge ni wa wananchi hivyo ni vema wananchi wakajitokeza katika maeneo ambayo mwenge utasimama ilikuweza kushiriki katika uzinduzi huo.

Dkt Anney ameongeza kuwa mwenge wa uhuru utakwenda kuzindu mradi wa vijana unaofahamika kwa jina la vijana mlimani blocks hivyo amewataka vijana kujiamini na kuachana na tabia ya kuchagua kazi ilikuweza kujikwamua kiuchumi na kuendelea kupata kipato .

Aidha amesema katika ujenzi wa miradi iliyojengwa kunafedha za uviko 19 na fedha za tozo Pamoja na mapato ya ndani ambazo zimetumika kujenga miradi itakayo zinduliwa na mwenge wa uhuru.

Mwenge wa uhuru katika wilaya ya Rungwe utazindua mradi ya maji Mpandapanda,mradi wa madarasa Ndembela one,bweni la wanafunzi chuo cha Ualimu Tukuyu,kikundi cha vijana Mlimani blocks,Jengo la wagonjwa wa dharura Makandana na mradi wa barabara Masebe- Lutete km 7.5