Chai FM

Mafunzo yawe chachu ya mabadiliko

22 November 2021, 9:36 am

RUNGWE-MBEYA

NA:STAMILY MWAKYOMA

Vijana wametakiwa kuwa vielelezo katika jamii kupitia mafunzo yanayotolewa na vyuo vya maendeleo ya wananchi hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na mgeni rasmi Ndugu Gerald Kimbunga  katika maafali ya 45 ya chuo cha maendeleo ya Wananchi Katumba (FDC)Wilayani Rungwe na kuwataka elimu walioipata ikawe chachu katika maendeleo ya taifa.

Wakizungumzia changamoto zilizopo chuoni hapo baadhi ya wanafunzi wamesema kuna changamoto zinazowakabili ikiwemo uhaba wa vifaa vya kujifunzia na wakufunzi kwa baadhi ya masomo na kuiomba Serikali kutatua changamoto hizo ili kuweza kupata elimu yenye tija.

Akijibu risala na changamoto mgeni rasmi  Kimbunga amemtaka Mkuu wa chuo kuandika andiko la uhitaji wa vifaa na wataweza kulitekeleza na changamoto zingine kuahidi kuendelea kushirikiana katika kuzitatua.

Nao wazazi walishiriki katika maafali hayo washukuru uongozi wa chuo kwakuweza kuwalea vijana katika maadili mema na kuweza kuleta mabadiliko kwenye jamii watakayoenda kuitumikia.