Chai FM

Rungwe yajinasua na maambukizi ya usubi

2 December 2023, 7:07 am

Baada ya kufanyika kwa tafiti mbalimbali kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa usubi mikoa ya nyanda za juu kusini jamii imehamasika na unywaji wa dawa na kuweza kutokomeza.

wadau mbalimbali wakiwemo watendaji wa kata,wenyeviti wa vijiji , madiwani,maafisa tarafa na madaktari

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Serikali imetangaza kusitisha utoaji wa kinga dawa za ugonjwa wa usubi kwa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, tangu mwaka 2022 baada ya kutoa dawa hizo kwa miaka 21 kutokana na mambukizi kupungua kwa watoto na kufikia asilimia 2 ukilinganisha na hapo awali.

Kauli hiyo imetolewa na Dr. Clara Mwansasu kutoka mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipao mbele wizara ya afya kwenye ufunguzi wa kufanya tathimini uliyofanyika shule ya sekondari Syelya kata ya Itete halmashauli ya Busokelo  ambapo amasema kutokana na utafiti uliyofanyika kwa ushirikiano na NIMR kulingana na utafiti huo utoaji wa dawa umesimamishwa hadi 2025.

kutoka wizara ya afya mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yalikuwa hayapewi kipaombele,Clara Mwansau akitoa maelekezo[picha na Lennox Mwamakula]

Katika hafla  ya utoaji wa hamasa ambayo  imewakutanisha viongozi wa serilikali kama vile watendaji wa vijiji,kata,madiwani maafisa tarafa na wenyeviji wa vijiji kwa dhumuni la kupeleka elimu kwa wananchi juu ya tafiti zilizofanyika kwenye maeneo yao juu ya ugonjwa wa usubi ulivyo pungua

sauti ya insert Dr clara

Kwa upande wake mgeni  rasmi kwenye mkutano huo wa kutoa hamasa mwenyekiti wa halmashauri ya Busokelo Anyosisye Njobelo ameishurukuru wizara ya afya kwa kushirikiana na NIMR kwa kuendelea kutoa elimu juu ya ugonjwa wa usubi kwani wananchi walikuwa hawafahamu na amesema miaka ya nyuma ugonjwa huo ulihusishwa na imani potovu.

sauti ya njobelo

Aidha nao baadhi ya watendaji walio hudhuria hafla hiyo wamesema wamepokea elimu hiyo na wanakwenda kuwa elimisha wananchi juu ya tafiti uliyofanyika na sababu zilizopelekea dawa kusitishwa kwa kipindi hiki

sauti ya Mtendaji

Sambamba na hilo naye mtakwimu kutoka Taasisi ya Taifa ya utafiti wa magongwjwa ya binadabu Hanifa kapera ametoa ushauri kwa wananchi kuendelea kutumia dawa zinazo tolewa na serikali kwani lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wake kuwa na afya bora na ameongeza kwa wazazi na walezi wawahimize watoto juu ya unywaji wa dawa.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Busokelo Anyosisye Njobelo akitoa neno la shukurani kwa wizara na NIMR[picha na Lennox mwamakula]

sauti ya mtakwimu