Chai FM

Jamii imetakiwa kusaidia watoto wenye uoni hafifu

15 November 2021, 3:09 pm

RUNGWE-MBEYA

Mwenyekiti wa chama wasioona (TLB )mkoa wa Mbeya ndg.YOHANA MONGA amewaomba wadau mbalimbali kote nchini kusaidia vifaa vya kufundishia watoto wenye mahitaji maalum mashuleni.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akikabidhi fimbo nyeupe kwa wanafunzi wasioona kwenye shule ya mahitaji maalum Katumba 2  iliyopo Wilayani Rungwe ambapo amekabidhi fimbo nane zenye thamani ya shilingi laki mbili.

Mwenyekiti  YOHANA MONGA amesema kutokana na vifaa Kupatikana kwa gharama chama cha watu wenye mahitaji maalumu Mkoa wa Mbeya jamii mzima inapaswa kuwa karibu na wanafunzi wenye mahitaji ili kuwaondolea changamoto wanazokumbana nazo mashuleni.

Kwa upande wao wanafunzi wameushukuru uongozi wa TLB Mkoa wa Mbeya kwakuwapatia fimbo hivzo kwani wamesema zinaenda kupunguza changamoto ya upungufu wa vifaa .

Nao walimu wa shu ya msingi katumba 2  wametoa shukurani zao za dhati kwa wanachama wote wa chama na watu wenye mahitaji maalumu na kuiomba Serikali kuwasaidia  vifaa mbalimbali kwani kutokana na ukosefu wa vifaa kama hivyi walimu wanakumbana na changamoto wakati wa kuwafundisha.