Chai FM

MH. ANTON MWANTONA ametoa vifaa ukarabati na ujenzi wa vyoo shule ya msingi Mabonde

22 April 2022, 1:03 pm

RUNGWE-MBEYA

Mbunge wa Jimbo la Rungwe MH. ANTON MWANTONA ametoa msaada wa vifaa kwa ajiri ya ukarabati na ujenzi wa vyoo katika shule ya msingi Mabonde iliyopo kata ya Msasani wilayani Rungwe.

Akimwakilisha Mbunge kukabidhi vifaa katibu wa mbunge wa jimbo la Rungwe ndg GABRIEL MWAKAGENDA amesema kuwa MH. Mbunge ameguswa na changamoto ya choo katika shule ya msingi Mabonde na kutoa vifaa ikiwa ni pamoja na saruji mifuko 18 ,tripu mbili za mchanga ,tripu moja ya kokoto na tofari,masinki ya vyoo ambapo jumla imeghalimu shilingi milioni moja na laki 6 .

Kwa upande wake diwani wa kata ya Msasani MH ROBIN MWAKAPESA ameishukuru ofisi ya mbunge kwa kuiona changamoto hiyo na kutoa msaada hali itakayoenda kuondoa tatizo hilo huku akishukuru miradi mbalimbali kupitia ofisi ya mbunge imeweza kufikiwa katika kata ya Msasani.

Sambamba na hayo walimu wa shule ya msingi Mabonde wametoa shukrani kwa mbunge wa jimbo la Rungwe MH ANTON MWANTONA kwa msaada kwani pindi ujenzi utakapokamilika wanafunzi wataweza kutumia vyoo na kuondokana na hali hatarishi ikiwa ni pamoja na magonjwa kutokana na uhaba wa matundu ya choo.