Chai FM

TOZO ya miamala ya simu yasaidia upatikanaji wa madarasa

10 September 2022, 9:26 am

RUNGWE-MBEYA

Kupitia TOZO ya miamala ya simu, Serikali imetoa jumla ya shilingi Million 12.5 kwa ajili ya ukamilishaji wa chumba Cha darasa katika shule ya Sekondari Ndembela one iliyopo kata ya Makandana.

Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imetoa kiasi Cha shilingi million 1,512,000/= na  nguvu za wananchi zenye thamani ya shilingi Million 6,117,000/= kwa ajili ya  ujenzi  wa chumba  hicho.

Chumba hiki kitazinduliwa na mbio za mwenge siku ya jumamosi tarehe 10.9.2022.

Katika Upande mwingine  shule ya Sekondari Iponjola, Itagata na Kalengo pia  zimenufaika na  mfuko wa TOZO na  kupokea kiasi Cha shilingi Million 12.5 kwa ajili ya ukamilishaji wa chumba kimoja Cha darasa kwa  kila shule na tayari vyumba vimekamilika.

Hata hivyo katika kuboresha afya ya jamii kupitia mfuko wa TOZO Serikali imetoa kiasi Cha shilingi million 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya Cha afya katika kata ya Ndanto.

Kituo kimefikia hatua nzuri na kukamilika kwake kutatoa fursa nzuri ya matibabu kwa karibu zaidi hasa  kwa mama na mtoto.

Serikali katika kuwajali wananchi wake pia kupitia mfuko wa TOZO imetoa kiasi Cha shilingi Million 105,532,000/= kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mwale- Ikama ililipo kata ya Masebe kukiwa ni kiungo muhimu Cha usafirishaji wa watu na Mali zao kutoka kata ya Mpata Halmashauri ya Busokelo na Masebe- Suma- Katumba Halmashauri ya Rungwe.