Chai FM

Mavazi yasiyo na staha yapigwa marufuku Rungwe

24 December 2023, 9:47 am

Mbunge wa jimbo la Rungwe Anthony Mwantona akijibu kero za wananchi.

Moja ya sababu iliyo tajwa kupolomoka kwa maadili ni pamoja na kuigwa kwa tamaduni za nje,hivyo jamii imeshauriwa kudumisha utamaduni wa maeneo yao.

Na lennox Mwamakula

Wananchi wa kijiji cha Mbaka kilichopo kata ya Kisiba wamemwomba Mbunge wa jimbo la Rungwe Anthony Mwantona kuwaruhusu vijana wa kike kuruhusiwa kuvaa suruali kutonakana na kupigwa marufuku kwa mavazi hayo kwa mtoto wa kike.

Wananchi wakiwasilisha kero kwa mbunge wao

Kilio hicho cha wananchi hao wamekiwasilisha mbele ya Mbunge wao alipofanya ziara ya kijiji kwa kijiji kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi ili aweze kuzitatua, akiwa kijiji cha Mbaka wakazi wa kijij hicho waliwasilisha kero mbalimbali kama vile ukosefu wa maji, umeme na uchakafu wa miundombinu ya barabara pamoja na suala pembejeo za kilimo.

sauti ya wananchi 1

Wakijibu kero hizo zilizowasilishwa na wananchi hao wataalamu wa idara mabalimbali alioambatana nao mbunge likiewmo suala la umeme msimamizi wa miradi ya REA wilaya ya Rungwe Ndg,Gwamaka Mwanjabeki  amesema  atafika kwenye kitongoji cha london ili kujua tatizo la baadhi ya watu kuosa umeme

sauti ya Gwamaka na Mbunge

Naye Tulinangwe Mwakipesile mkazi wa kijiji cha mbaka amemuomba mbunge Mwantona kuwa ruhusu vijana wa kike kuvaa suluali kama awali kwani mabinti hao wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazo onyesha viongo vya  sehemu za mili yao

sauti wananchi 2

Akijibu kero hiyo chifu Joeli Mwakatumbula amesema suala la kuruhusu mabinti kuvaa suluali ni uvunjaji wa tamaduni za mwafirika hiyo amesema hata ruhusu maadili kupolomoka ataendelea kulinda tamaduni  za mwafika

Chifu mwakatumbula akizunguzia suala la maadili kwa vijana

sauti ya chifu 1

Mwakatumbula amesema kitendo cha Kuruhusu mabinti kuvaa mavazi yasiyo kuwa na staha kunasababisha kuwepo kwa vitendo vya ubakaiji na kuwasingizia watu kuwa wamewabaka kutokana na mavazi yao amesema atalisimamia hilo hataruhusu vijana kuvaa suluali ndani ya wilaya mzima

sauti ya chifu 2