Chai FM

Wananchi wamshukuru Rais Samia fedha ujenzi shule ya sekondari

20 February 2022, 5:08 pm

RUNGWE-MBEYA

Umoja na ushirikiano  wa wakazi wa kata ya Msasani wilayani Rungwe umetajwa kuwa chanzo cha kumalizwa kwa ujenzi wa shule ya sekondari Msasani inayojengwa katika mtaa wa Bulongwe.

Ameyasema hayo diwani wa kata ya msasani mh ROBIN MWAKAPESA, wakati wa maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo ambapo ameanza kwa kuwaomba wananchi kuongeza ushirikiano na umoja kwani kwa kufanya hivyo kutapelekea kumaliza ujenzi huo kwa mda husika.

Aidha MWAKAPESA ameongeza kwa kuwaasa wakazi wa msasani kuachana na siasa ambazo hazina maendeleo kwao na zaidi siasa hizo zitapelekea kurudisha nyuma maendeleo ya kata yao ya msasani.

STEVEN  MWAKINDOPA na AMANI MWAKEJA, ni baadhi ya viongozi katika kata ya Msasani kwa upande wao wameishukuru serikali ya awamu ya sita ya Mh Samia Suluhu Hassan, kwa kuwasaidia kiasi cha shilingi  milion 500, ambazo zitakwenda kuunga mkono juhudi za wananchi katika ujenzi wa shule hiyo.

Sambamba na hayo nao wananchi wameahidi kuendelea kuonesha juhudi za umoja ili shule hiyo iweze kukamilika kwa wakati kwa ujenzi wa shule hiyo kwani  kilikuwa ni kilio chao cha muda mrefu na kitakwenda kupunguza adha waliyokuwa wakiipata watoto wao kwa mda mrefu.

Ujenzi wa shule hiyo unategemewa kumalizika kufikia april 11, 2022 kutokana na makubaliano baina ya wananchi na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe, na kukamilika kwa shule hiyo utakwenda kupunguza adha ya watoto waliokuwa wakitembea umbali mrefu kwenda kupata huduma ya masomo.