Chai FM

Polisi kukabiliana na vitendo vya kikatili Rungwe

29 November 2023, 8:54 am

ili kuweza kutokomeza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia ikiwa ni pamoja na ukatili kwa wanawake na watoto jamii imetakiwa kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa kwenye vyombo vya kisheria.

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Jamii imeshauriwa kuachana na vitendo vyaa kikatili vinavyo sababisha  vifo na kupelekea kuacha familia hasa watoto kuishi kwenye mazingira magumu

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa usalama Barabarani kutoa jeshi la polisi wilayani Rungwe  Felix Kakolanya kwenye  mkutano wa hadhara uliyo fanyika kjiji cha kawetele chini kata ya kawetele wilayani Rungwe ambapo amesema kuna madhara makubwa kwa mzazi anaye fanyiwa pamoja na  mtoto ikiwa ni kuthirika kiakili.

sauti ya kakolanya o1

Aidha Kakolanya  amesema kumekuwepo na vifo vingi wilayani Rungwe kutokana na baaadhi ya watumiaji wa Barabara  hasa watembea kwa miguu kutofuata sheria  zilizopo na wengine kuvuka Barabara wakiwa wamelewa kitendo kinacho changia mtu kugongwa na kupotenza  uhai.

Mkuu wa kitengo cha usalama Barabarani wilayani Rungwe Felix Kakolanya [Picha na Lennox Mwamakula]

Hivyo amewaomba wananchi kwa kipindi hiki cha mwisho mwa mwaka kutumia barabara vizuri na amesema wauzaji wa pombe za kienyeji wafuate muda ulipangwa wa kufungua biashara zao kwani operesheni maalum ya kuwachukulia hatua za kisheria inaanza

sauti ya kakolanya o2

Kwa upande wake mkuu wa kituo cha polisi Tukuyu Asp Raphael Mlangwa amesema watoto wanafanyiwa vitendo mbalimbali vya kikatili likiwemo suala ulawiti kwa watoto kushamili hivyo amewasihi wazazi na walezi kuwa karibu  watoto ili kukabiliana na vitendo vya ukatili vilivyopo ndani ya jamii.

sauti ya mkuu wa kituo

Naye mwenyekiti wa kijiji cha kawetele chini  Alphonce Mwabulambo amewaomba wakazi wa kawetele kutoa taarifa ya vitendo vya kiharifu Kama vile uwizi wa kuku,Bata na Nguruwe vinavyo endelea kijijini hapo ili wahusika wachukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwenye vyombo vya kisheria

Mkuu wa kituo cha polisi Tukuyu ASP Raphael Mlangwa [picha na Lennox Mwamakula]

sauti ya mwenyekiti

Sambamba  na hilo jeshi la polisi wilayani Rungwe wananchi kugombaniana ardhi kwani kumekuwepo na kesi nyingi za migogoro ya ardhi vitendo kinacho pelekea kuuana na kutoelewana kwenye famila na jamii kwa ujmla

sauti ya jeshi la polisi