Chai FM

Tozo za maegesho zawakwamisha bodaboda

21 November 2023, 3:17 pm

RUNGWE-MBEYA

Sheria ndogo zinazopitishwa kwenye vikao vya mabaraza ya madiwani kukwamisha baadhi ya shughuli za kimaendeleo kwenye maeneo husika.

Na Lennox mwamakula

Kutokana na kuwepo kwa kamatakamata ya vyombo vya moto na kutozwa faini ya maegesho waendesha pikipiki maarufu bodadoda wilayani Rungwe wameiomba serikali kuwaondolea faini wanayo tozwa na Mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini LATRA.

Wametoa ombi hilo mbele ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera alipofanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi wilayani Rungwe ambapo Bodaboda hao wamesema wameshangazwa na kitendo cha Mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini LATRA kuwatoza faini kuanzia shilingi laki mbili hadi million moja pindi wanapo shindwa kulipa shilingi 17,000 iliyowekwa kwa mujibu wa sheria.

sauti za Bodaboda

Kwa upande wao LATRA wamesema kiasi hicho cha pesa wanacho tozwa ni kwa mujibu wa sheria ndogo walizo jiwekea ndani ya Halmashauri pindi mwendesha chombo hicho anapo kamatwa na hajalipa fedha kiasi cha shilingi elfu kumi na saba ndani ya muda.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya akitoa tamko juu ya waendesha pikipiki [picha na Lennox]

sauti ya Latra

Baadhi ya viongozi alioambatana nao mkuu wa mkoa akiwemo mwenyekiti wa  mtaa wa Bulyaga na mbunge wa viti maalumu Suma Fyandomo wamemuomba mkuu wa mkoa kuona namna ya kuwasaidia kwani gharama wanayotozwa ni kubwa kulingana na kipato chao.

sauti za viongozi

Aidha Mkuu wa mkoa ameitaka halmashauri ya Rungwe kuona namna ya kufanya marekebisho ya sheria kwani faini wanayo tozwa ni kubwa ukilinganisha na kazi yao na kuagiza LATRA kuwapatia pikipiki zao ili waweze kuendelea na shuguli za kujiingizia kipato

sauti ya Mkuu wa mkoa