Chai FM

Wanafunzi kumaliza vitendo vya ukatili shuleni

26 April 2024, 2:59 pm

Vijana wametakiwa kuwa msitari wa mbele kutoa taarifa oindi wanapo fanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia

MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Kutokana na ongezeko la vitendo vya ukatili vinavyoripotiwa kwenye maeneo mbalimbali mkoani mbeya, serikali kwa kushrikiana na wadau mbalimbali wamekutana ili kuboresha mifumo ya kupinga ukatili pamoja na kuzindua madawati wa kupinga vitendo hivyo shuleni.

wanafunzi wakiwa na walimu wakikabidhiwa vifaa vya michezo

Imeelezwa kuwa lengo la kuundwa kwa madawati hayo ni kutokomeza ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili kwa watoto ili waweze kujadili kwa pamoja vitendo hivyo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa dawati la kupinga vitendo vya ukatili ndani ya shule ya sekondari Ihanga, Amos Mpili ambaye ni afisa maendeleo ya jamii kutoka wizara ya maendeleo ya jamii jinsia, wanawake na makundi maalumu amesema kuwa kuundwa kwa dawati hilo kutachangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa vitendo vya ukatili ili waweze kutimiza malengo yao.

sauti ya afisa maendeleo

Mpili amemuagiza mkuu wa shule kuandaa utaratibu wa kupata sanduku la maoni na kuwekwa sehemu rafiki ili kuwarahisishia wanafunzi kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili vinavyofanywa shuleni hapo na nje ya shule ili waweze kusaidiwa kwa wakati.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Ihanga Agrey Masebo amepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali na wadau mbalimbali zinazokusudia kupunguza vitendoo vya ukatili mashuleni huku akiahidi kutumia kwa malengo Televisheni, Spika, jezi na mipira iliyotolea shuleni hapo.

sauti ya mkuu wa shule ya sekondari ihanga

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa kuongoza madawati ya ukatili pamoja na mwalimu wa malezi shuleni hapo wameahidi kutoa ushirikiano kwa waathirika wa vitendo vya ukatili na kuhakikisha elimu inaendelea kutolewa ili kutokomeza vitendo hivyo.     

sauti za wanafunzi