Chai FM

Billioni 26.9 kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo 2024/2025 Busokelo

19 January 2024, 11:31 am

Na mwandishi wetu

Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo imepanga kutumia shilingi bilioni 26.6 kwa mwaka fedha 2024/2025.

Hayo yameleezwa katika kikao cha Baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri tarehe 18/01/2024 kwaajili ya kujadili mapendekezo ya Mpango na Bajeti  mwaka wa fedha 2024/2025.

Akiwasilisha Mapendekezo ya Bajeti katika Baraza hilo, Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu Bw. Chrispin Mng’anya amesema kuwa Katika mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri inatarajia kukusanyanya na kupokea jumala ya shilingi Bilioni 26.9 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato, ikwemo mapato ya ndani shilingi bilioni 2 sawa na asilimia 7.42 na ruzuku kutoka serikali kuu ni shilingi bilioni 24.9 sawa na asilimia 92.58. 

Vipaumbele katika bajeti hii ni utekelezaji na ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikwemo Elimu, Afya, Kilimo na mifugo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Mhe. Anyosisye Njobelo ametangaza kupitishwa kwa Mapaendekezo ya Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 yenye jumla ya shilingi bilioni 26.9, huku akisisitiza uadilifu na ushirikiano baina ya Wananchi, Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu wa Halmashauri katika utekelezaji na usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya Umma.

Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Bw.Christoper Nyambaza, amepongeza Baraza la Madiwani na Wataalamu wa Halmashauri kwa kuanzisha mchakato wa Bajeti tangu hatua za wali hadi kufikia katika Baraza  kwa kuzingatia kipaumbele zaida katika ukamilishaji miradi  inayoendelea. Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo imeaandaa Mapendekezo ya Mpango na Bajeti  2024/2025 kwa kuzingatia miongozo mbalimbali ya upangaji bajeti kama vile Dira ya maendeleo  ya mwaka 2025, Malengo ya Maendeleo endelevu (SDGs) , Mpango wa Maendeleo wa tatu wa miaka mitano (FYDP) ilani ya uchaguzi Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020.