Chai FM

Wanunuzi parachichi wafuate bei elekezi ya serikali

22 March 2022, 8:47 am

RUNGWE-MBEYA

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe MPOKIGWA MWANKUGA amewataka wakulima wa zao la parachichi kuuza zao hilo kwa kufuta bei elekezi iliyotolewa na serikali ya shilingi 1600 kwa kilo.

Ametoa kauli hiyo alipo kuwa akitoa elimu kwa wananchi na wakulima wa zao hilo nakusema kuwa kutokana na malalamiko yaliyopo ya kutokuwepo kwa wanunuzi serikali imeweka mpango nzuri wa kumnufaisha mkulima kwa lengo la mtaka mnunuzi kununua zao hilo kwa kupitia AMCOS.

Hata hivyo Mwankuga amewaomba  wanunuzi,wakulima pamoja na vyama vya ushirika washirikiane na serikali ili kusukuma maendeleo ya halmashauri ya Rungwe na kukuza kipato cha mkulima wa zao la parachichi

Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe MPOKIGWA MWANKUGA amesema kama kuna changamoto yoyote kwa wanunuzi wa zao la parachichi  halmashauri iko tayari kusikiliza changamoto hizo ili ziweze kutatuliwa,na amewaomba wakulima kulima kwa kufuata maelekezo yanatolewa na wataalamu ili kulima kilimo chenye tija.