Chai FM

TANLAP yawajengea uwezo wasaidizi wa kisheria Rungwe

23 November 2021, 9:34 am

RUNGWE

Kaimu mkurugenzi kutoka mtandao wa Mashirika yanayotoa msaada wa kisheria Tanzania [TANLAP] MCHELELI MACHUMBANA ameitaka jamii kujua sheria mbambali ili kukabiliana na unyanyasaji uliopo kwenye maeneo yao.

Ametoa kauli hiyo mbele ya wasaidizi wa kisheria waliopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya  wakati wa kuwajengea uwezo wa namna ya utoaji elimu ya kisheria kwenye kata tano zilizo kuwa kwenye mpango katika awamu hii.

Machumbana amesema lengo la mradi huu wa mwanamke mwanamke imara ni kumkinga mwanamke nav itendo vya ukatili wa kijinsia katika njia mbalimbali ikiwemo kuwawezesha kiuchumi, kuwawezesha kufikia ngazi za maamuzi na kuwawezesha kufikia haki.

Naye mratibu na mfutiliaji wa mradi kutoka taasisi ya wasaidizi wa kisheria Rungwe legeland  socialwelfare EDDIE MWANGALABA amesema kutokana na mafunzo waliyopatiwa wamejifunza namna ya kuihudumia jamii juu ya masuala ya kisheria kama vile migoro ya ardhi na ukatili wa kijinsia.

Aidha Mwangalaba ameiomba jamii Kuanzia ngazi ya vitongoji ,vijiji na kata kutoa ushirikiano kwa wasaidizi wa kisheria waliopo kwenye maeneo yao ili kukabiliana na changamoto iliyopo ngazi hiyo ya chini

Kwa upande wao baadhi ya washiriki waliohudhuria mafunzo hayo wamesema wataenda kutoa elimu kwa wananchi kama ilivyo kusudiwa na wameomba wananchi kutoa ushirikiano kwao pale ambapo wanakwama kisheria ili waweze kusaidiwa.

Ikumbukwe kuwa wilaya ambazo zimepitiwa na mradi huu wamwanamke imara katika mkoa wa mbeya ni wilaya ya MBARALI na Rungwe na ndani ya Rungwe jumla ya kata tano ndizo ambazo zimepitiwa na mradi.