Chai FM

Wakulima wa parachichi walia na walanguzi Rungwe

6 June 2024, 9:23 am

Makampuni yanayo nunua parachichi yamaeonywa kufutiwa vibali kutoka na tabia iliyop ya kuto walipa wakulima fedha zao kwa wakati

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya wakulima wa zao la parachichi kuto lipwa fedha zao serikali imeagiza kukamatwa kwa mnunuzi  wa parachichi wa kampuni la mbembati ili aweze kuwalipa wakulima hao.

Agizo hilo la serkali limetolewa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera alipokuwa akisikiliza kero za wananchi wa wilaya Rungwe  kwenye viwanja vya stendi mpya ya mabasi

Issa andengulile Nsamuli ni moja wa wakulima ambaye ajalibwa fedha zake kiasi cha Shilingi milioni tano na laki saba tangu parachichi zake zilipo chukuliwa na mnunuzi huyo

wananchi wakitota kero mbele ya mkuu wa mkoa

sauti ya mkulima ndg Isaa Nsamuli

Mkuu huyo wa mkoa ameshangazwa na afisa kilimo wa wilaya ya Rungwe kutokuwa makini na usimamizi wa zao la parachichi na kuwanyumbisha wakulima kwa kuto walipa fedha zao

sauti ya Mkuu wa mkoa 1

Aidha  Homera ametoa maelekezo kwa ocd wa wilaya aweze kumtafuta kokote aliko Mwenye kampuni hilo la mbebati ili aweze kuwalipa wakulima wote wanao mdai  ndani ya masaa sabini na mbili

sauti ya Mkuu wa mkoa 2

Sambaba na hilo mkuu wa mkoa amesema makampuni anayo chukua parachichi kwa wananchi bila kulipa halmashauri waone namna ya kuwafutia vibali vya kuendelea kununua parachichi ndani ya wilaya ya Rungwe