Chai FM

Wakazi wa Ilenge wilayani Rungwe wafurahia kupata zahanati

7 January 2024, 12:32 pm

Baada ya kufuata huduma ya matibabu umbali mrefu wananchi wa kijiji cha Ilenge wameipongeza serikali kwa kuwajengea zahanati kwani wamesema imewapunguzia changamoto ya kukosa matibabu.

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Mkuu wa wilaya Rungwe Jaffar Haniu amepongeza juhudi zilizofanya na wakazi wa kijiji cha ilenge kata ya kyimo wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa kujenga zahanati kwa nguvu zao.

Kauli hiyo ameitoa kwenye hafla ya uzinduzi wa zahanati hiyo imeifanyika kwenye  uwanja wa  zahanati hiyo amesesema kutokana na jitihata walizo nazo wanchi hao serikali itaendelea kuwaunga mkono kwa kila hatua watakazo kuwa wakiziffanya kwenye kata yao

wananchi wa kijiji cha ilenge wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa zahanati [picha na Lennox Mwamakula]

Awali akisoma taarifa ya ukamilishaji wa ujenzi mganga mfawidhi wa zahanati hiyo Musa Gwenoi amesema ujenzi wa zahanati ulianza ujengwa tangu mwaka 2014 kwa nguvu za wananchi na katika mwaka wa fedha wa mwaka 2021/2022 zahanati ilipata fedha kiasi cha shilingi million Hamsini  kwaajili ya ukamilishaji

Sauti ya mganga mfawidhi 1

Hata hivyo Gwenei amezitaja changamoto zinazo ikabili zahanati hiyo kuwa ni kukosenana kwa vifaa mbalimbali kama feniture pamoja na nyumbaza watumishi ili kuwaondolea watumishi kukaa mbali na sehemu ya kazi

mgamga mfawidhi wa zahanati ya ilenge akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi

sauti ya mganga mfawidhi 2

Akijibu taarifa hiyio mkuu wa wilaya ya Rungwe mh,Jaffar Haniu amesema wananchi washirikiane vizuri na wataalamu wa afya waliopelekwa katika zahanati hiyo kwani lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wnapata huduma wakati wote na ammtaka mrugenzi kutenga fedha za mapato ya ndani ili samani zinunuliwe kwa matumizi ya zahati ya ilenge

mkuu wa wilaya ya Rungwe Jafarr Haniu akizungumza mbele ya wananchi wa kijiji cha ilenge wakiti wa uzinduzi wa zahanati ya ilenge

sauti ya mkuu wa wilaya 1

Haniu amesema kutokana na ubofu wa barabara ya kuelekea kwenye zahanati hiyo amemwagiza meneja wa Tarura wilaya ya Rungwe kuakikisha barabara hiyo inakarabatiwa vizuri ili iweze kupitika kwa urahisi

Sauti ya mkuu wa wilaya 2

Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha ilenge  wameishukuru serikali kwa kuwaunga mkono kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo kwani wamesema walikuwa wakisumbuka kufuata huduma ya afya umbali mrefu

sauti za wananchi