Chai FM

Jumla ya watoto 61125 kupata chanjo Rungwe

28 February 2024, 6:46 pm

Ili kuhakikisha mtoto analindwa na magonjwa yasiyopewa kipaombele, jamii inatakiwa kuwa mstari wa mbele kujitokeza kuwapatia chanjo.

Na lennox Mwamakula

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Hanniu ameiomba jamii kutoa ushirikiano kwa  walimu wanaowahudumia  watoto wenye mahitaji maalum ili watoto waweze kufikia ndoto zao

Ametoa kauli hiyo kwenye uzinduzi wa utoaji wa dawa kinga za kichocho na minyoo kwa watoto wenye umri wa kuazia miaka mitano hadi kumi na nne uzinduzi uliofanyika kwenye  viwanja vya shule ya msingi katumba II iliyopo kata ya Ibighi amesema chanjo hiyo ni salama na haina madhara yoyote

Mkuu wa wilaya jaffar Hanniu akimpaitia mmoja wa wanafunzi vidonge

sauti ya mkuu wa wilaya 1

Hata hivyo Hanniu amesema halmashauri ya wilaya ya Rungwe jumla ya watoto wanaotarajiwa kupatiwa kinga tiba ni takribani watoto 61,125 lengo ni kuboreha afya za watoto kwa ujmla

Mganga mkuu wa hospital ya wilaya ya Rungwe [Kushoto] akiwa na mratibu wa chanjo wakitoa maelekezo mbele ya mkuu wa wilaya[picha na Lennox Mwamakula]

sauti ya mkuu wa wilaya 2

Kwa upande  wake mratibu  wa magonjwa yasiyo pewa kipao mbele Leonard Shaba amesema zoezi limeratibiwa vizuri kuhakikisha watoto wote wanafikiwa na kupatiwa chanjo hiyo.

sautit ya mratibu 1

Aidha mratibu huyo amesema serikali imegharamia kutoa chanjo hizo ili kila mtoto apate kinga tiba hizo bila gharama yoyote.

sauti ya mratibu 2

Naye mwalimu wa afya kutoka shule ya msingi Katumba II Andrew  Ngewele amesema zoezi la kuwapatia chanjo watoto limeenda vizuri na hakuna madhara yaliyo jitokeza huku watoto wakifurahia chanjo hiyo .

sauti ya mwalimu