Chai FM

Taulo zimekuwa mkombozi kwa wanafunzi wa kike mashuleni

30 September 2023, 3:04 pm

wanafunzi wa shule ya sekondari tukuyu wilayani Rungwe wakiwa wanapokea taulo[picha na lennox mwamakula]

jamii imetakiwa kuendelea kumsaidia mtoto wa kike ili aweze kuondokana na vikwazo vinavyoweza kumkwamisha kutimiza ndoto zake

RUNGWE-MBEYA

Na lennox mwamakula

Jumla ya pisi elfu ishirini za taulo za kike za softcare zimetolewa na mbunge wa viti maalumu Sophia Mwakagenda kwa wanafunzi wa kike 279 wa kidato cha kwanza mpaka kidato cha sita.

Mbunge viti maalum Sophia Mwakagenda akikabidhi taulo za kike kwa wanafunzi[picha na lennox mwamakula]

Akizungumza na wanafunzi shule ya sekondari Tukuyu Mwakagenda amesema kuwa wameamua kugawa taulo hizo kwa wanafunzi wa kike kutokana na kushindwa kuhudhuria masomo yao wakati wa hedhi kutokana na kukosa taulo hizo.

sauti ya mwakagenda 1

Amesema kuwa kwa kushirikiana na kampuni ya Duwi care watengenezaji wa taulo za kike za soft care wamedhamiria kuifikia mikoa yote ya nyanda za juu kusini na watazifikia jumla ya shule 306.

sauti ya mwakagenda 2

Kwa upande wake Emmanuel Kiula afisa msimamizi wa masoko kutoka kampuni ya Duwi care amesema kwa ushirikiano na mbunge wa viti maalumu wamekabidhi taulo za kike zenye thamani ya shilingi million moja, laki moja na elfu nne ili kutatua changamoto ya watoto wa kike kukosa masomo kutokana na hedhi.

sauti ya emmanuel

Akizungumza kwaniaba ya walimu wa shule ya sekondari tukuyu, Mwalimu Riziki amemshukuru mbunge wa viti maalumu  Sophia Mwakagenda kwakufika shuleni hapo na kukabidhi taulo za kike ambazo ni muhimu kwa kila mtoto wa kike, huku akiwaomba wanawake wengine kuwaaidia katika mahitaji mbalimbali kwaajili ya wanafunzi.

sauti ya mwalimu Riziki

Akitoa shukrani mara baada ya kupokea taulo za kike Herena Lupogo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha sita shuleni hapo ameahidi kwaniaba ya wanafunzi wenginem kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.

sauti ya mwanafunzi