Hii ni shule ya Msingi Nuru iliyopo Kata ya Bagamoyo Tukuyu Mjini yenye mchepuo wa kingereza ambayo inatajwa kupanua maarifa na ujuzi kwa wanafunzi wa Wilaya Ya Rungwe
Kupitia Mapato ya shule hii pamoja na vyanzo vingine, Halmashauri imeweza kujenga na kusajili shule nyingine mpya kwa mchepuo wa Kingereza katika kata ya Kyimo (Umoja English Medium) na Ushirika Eng medium iliyopo kata ya Mpuguso.