Chai FM

Milioni 362 kujenga stendi ya vumbi Tukuyu mjini

21 September 2023, 4:08 pm

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Bw. Lenatus Mchau akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake. ( picha na Judith Mwakibibi)

Kukamilika kwa stendi ya vumbi maarufu kama stendi ya Noah Tukuyu mjini itakuwa chachu ya maendeleo kwani itaondoa adha ya watumiaji wa stendi hiyo kwa msimu wa masika na kiangazi.

Na Lennox Mwamakula – Rungwe-Mbeya
Jumla ya shilingi milioni 362 zimetengwa na halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwaajili ya ujenzi wa stendi ya Vumbi maarufu stendi ya Noa iliyopo Tukuyu mjini.
Kauli hiyo imetolewa na mkurugengenzi mtendaji Renatus Mchau alipo kuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema kutokana na changamoto iliyokuwepo kwa muda mrefu kwenye stendi hiyo halmashauri imeamua kuitatua ili shughuli za kiuchumi ziendelee.

Sauti ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Rungwe Renatus Mchau

Hata hivyo Mchau amewaomba wananchi wanao fanya biashara zao kwenye eneo la stendi kufuata utaratibu ulio wekwa ili kukamilisha zoezi la ujenzi wa stendi hiyo kwa muda ulio pangwa.

Sauti ya Mchau mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe

Sambamba na hilo amesema ujenzi wa stendi hiyo unatarajiwa kukamika mwishoni mwa mwezi wa kumi mwaka huu na kuanza kutumika hivyo watumiaji wa stendi hiyo wametakiwa kuwa wavumilivu kwa kipindi chote ambacho ujenzi unaendelea.

Sauti kukamilika kwa stendi

Baadhi ya wafanyabiashara kwenye eneo hilo la stendi wameushukuru uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa kuboresha stendi hiyo kwani wamesema inaenda kuinua uchumi wa watumiaji pamoja na kuongeza pato ya halmashauri.

Sauti za wananchi kuhusu stendi ya vumbi

Stendi ya vumbi maarufu kama stendi ya Noah Tukuyu mjini ni miongoni mwa miradi sita iliyokaguliwa na mwenge wa uhuru mwaka huu 2023 na ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi octoba 2023