Chai FM

Vitabu zaidi ya elfu tatu vyapokelewa Rungwe

16 December 2021, 2:27 pm

RUNGWE.

Katika kuboresha mazingira ya elimu nchini wadau mbalimbali wa elimu wameshauriwa kusaidia vifaa mbalimbali kama vile vitabu vya kiada na ziada.

Akizungumza mara baada ya kupokea vitabu kutokea taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Sakyambo interprisess yenye makao makuu yake jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya Renatus Mchau amesema kwamba halmashauri ilikuwa na upungufu wa vitabu katika maktaba za shule hivyo vitabu hivyo vitasaidia wanafunzi kujiongezea maarifa zaidi.

Kushoto ni mdau wa elimu Rungwe kutoka shirika lisilo la kiserikali la Sakyambo interprisess Bw. Clement akimkabidhi vitabu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Bw. Renatus Mchau

Bw. Monangi kilembe ni kiongozi wa taasisi hiyo amesema kwamba tangu mwaka 2011 wamekuwa wakifanya kazi hapa nchini huku wakiishukuru halmashauri ya Rungwe kwa namna walivyo wapokea vizuri ukilinganisha na halmashauri zingine.

Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mh. Mpokigwa Mwankuga ameishukuru taasisi hiyo huku akimuagiza mkurugenzi kukusanya na kurejesha vitabu vyote ambavyo havitumiki katika silabasi ya kama vile vitabu vya lugha ya Kireno.

kulia ni mgeni rasmi bw. mpokigwa mwankuga ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Rungwe akipokea vitabu kutoka kwa Bw. Clement

Mwl Nyimbo Mikosi ni mwalimu wa shule ya sekondari Bulyaga wilayani hapa akizungumza kwa niaba ya walimu waliokabidhiwa vitabu hivyo ameishukuru taasisi ya Sakyambo interprisess kwa msaada huo kwani ni vitabu vitakavyo waongezea maarifa zaidi wanafunzi.

INSERT MWALIMU……………….

Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo wameishukuru serikali kuruhusu mdau huyo a elimu kusaidia katika sekta ya elimu kwani kumekuwa na changamoto ya vitabu vya kujiongezea maarifa katika shule zao.

INSERT WANAFUNZI………………..

baadhi ya wanafunzi na walimu wakikagua vitabu

Taasisi ya Sakyambo interprisess imelenga kuisaidia jamii katika sekta ya elimu ambapo hadi sasa ni wilaya saba katikia mikoa tofauti hapa nchini imeishanufaika kupitia taasisi hiyo.

Miongoni mwa wilaya hizo ni pamoja na Rungwe, moshi na Kibiti ambayo ni wilaya ya kwanza kusaidiwa na taasisi hiyo.