Chai FM

Wanawake wahimizwa kushiriki ngazi za uongozi

8 March 2024, 4:17 pm

Baadhi ya wanawake wakisheherekea siku ya mwanamke duniani (picha na Judith Mwakibibi)

Ili kuhakikisha uchumi wa familia unaimarika, wanawake wametakiwa kutambua nafasi zao kwenye jamii.

Serikal imetakiwa kuhakikisha inaendelea kuwakwamua wanawake kiuchumi na kijamii ili kuweza kufikia maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Katibu tawala wa wilaya ya Rungwe Ally Kiumwa akizungumza kweye Siku ya Wanamke Duniani [picha na Judith Mwakibibi]

Wito huo umetolewa na  mwenyekiti wa jukwaa la wanawake  wa wilaya  Rungwe Lusa Mwankenja wakati wa sherehe ya Siku ya Mwanamke iliyofanyika katika ukumbi wa Mwankenja.

Sauti ya mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Rungwe

Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi katibu tawala wilaya ya Rungwe Ally Kiumwa amesema ni vema wanawake kuendelea kushikamana katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushiri katika nafasi za uongozi pindi zinapokuwa zinajitokeza katika jamii kwani kidole kimoja hakivunji chawa.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi halmashauri ya Rungwe Castor Makeula amesema halmashauri inatambua mchango wa wanawake kama  halmashauri wameendelea kutoa mikopo kwa wanawake bila riba ili kuhakikisha mwanamke anajikwamua kiuchumi katika shughuli za maendeleo kupitia mikopo ambayo inatolewa.

Sauti ya kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe.

Kwa upande wao wadau waliojitokeza katika shughuli hiyo ya wanawake wakiwemo shirika la Care International mratibu wa mradi huo Mwanane Madebo amesema wao wamekuwa wakitoa elimu kwa wanawake ili waendelee kupata mikopo kwa kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali na  kujikwamua kiuchumi.

Sauti ya baadhi ya wadau walioshiriki maadhimisho ya siku ya mwanamke.

Siku ya mwanamke huadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka ambapo maadhimisho hayo kwa mkoa wa Mbeya yamefanyika katika wilaya ya Mbarali yakiwa na kauli mbiu “Wekeza kwa wanawake kurahisisha maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii”.