Chai FM

Kukosekana kwa wosia chanzo cha migogoro ya ardhi

12 September 2023, 8:11 am

Utamaduni wa watu wengi kutoandika wosia imetajwa kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi katika jamii nyingi nchini Tanzania huku mila na desturi zikitajwa.

Na Lennox Mwamakula- Rungwe

Jamii imeshauriwa kuwa na utaratibu wa kuandika wosia ili kuondokana na mkanganyiko juu ya masuala ya uharali wa umiliki wa mali mbalimbali ikiwemo kuondoa migogoro ya ardhi inayo nyima nafasi wanamke wa kinyakyusa umiliki ardhi.

awali ilikuwa vigumu kumlikisha mwanawake ardhi kutokana na dhana ya kuwa mwanamke ataolewa na kumilikishwa kwa mumewe.

Kauli hiyo imetolewa na mwanasheria BRIGHTER SHAO kutoka chama cha wanasheria wanawake Tanzania akizungumza na kituo hiki amesema kwa muujibu wa sheria ya mwaka 1999 na iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 imeweka usawa kwa mtu nyeyote kumiliki ardhi na amsema njia nzuri ya kuondoa migogo ya ardhi jamii ikumbuke kwandika wosia.

Sauti ya mwanasheria

Kwaupande wao wazee wamesema hapo awali ilikuwa vigumu kumlikisha mwanawake ardhi kutokana na dhana ya kuwa mwanamke ataolewa na kumilikishwa kwa mumewe hivyo wanawake wametakiwa kujitambua na kujua haki zao

Sauti ya wazee

Hata hivyo nao baadhi ya wananchi wamesema mila ya kinyakyusa ya kutomilikisha mwanamke ardhi ni sahihi kwasababu mwanamke ataolewa na kwenda kumilikishwa ardhi sehemu alio olewa

sauti za wananchi

Mwanasheria DANI SANDE kutoka shirika lisilo la kiserikali la [SAUTI YA HAKI TANZANIA] amesema wamekuwa wakikumbana na kesi nyingi ofisini kwao zinazo husu masuala ya ardhi,na ameitaka jamii ya kinyakyusa kuondokana na mawazo hasi juu ya umilikishwaji wa ardhi kwa mwanamke.

Sauti ya Dani Sande wa sauti ya haki Tanzania