Chai FM

Vijana jitokezeni kupima mambukizi ya ukimwi Rungwe

21 March 2024, 12:13 pm

Mratibu wa ukimwi Rungwe Bw,George Mashimbi[picha na Yona kibona]

Katika kuhakikisha jamii inakuwa salama, vijana wameshauriwa kuwa msitari wa mbele kujua afya kwani ndilo kundi linalotegemewa katika ujenzi wa taifa.

RUNGWE-MBEYA

Na lennox mwamakula

Imeelezwa kuwa jumla ya wakazi 12,158 wilayani Rungwe mkoani Mbeya wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWIkati ya hao wakazi 659 ni vijana huku wanawake wakiwa 467 na wavulana 192.

Takwimu hizo zimetolewa na Mratibu  wa UKIMWI Halmasahauri ya Rungwe Bwana George Mashimba katika kikao kilichowakutanisha vijana na mtandao wa wanawake wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania.

Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe wa John Mwankeja siku ya jumanne ya tarehe 20 mwezi march mwaka 2024 kwa dhumuni ya kutoa elimu kwa vijana juu ya maambukizi ya virus vya UKIMWI.

Kaimu mkurugenzi akitoa maelekezo kwa vijana walioshiriki mafunzo [picha na yona kibona]

Mtandao wa Wanawake  wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (National Networking Women Living With HIV in Tanzania) umewakutanisha vijana mashujaa wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo kutoka katika vijiji sita katika kata ya Kisondela, Kyimo, Isongole, Makandana, na  Ndanto.

sauti ya mratibu wa ukimwi Rungwe

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Rungwe bi,ndelwa ameomba vijana kujenga tabia ya kupima afya zao kwani kunasaidia kujiamini na kuendelea kufanya shughuli zako bila wasiwai hata kama utakuta umeambukizwa

Baadhi ya washiriki mafunzo hayo ya elimu juu ya mambukidhi ya virusi vya ukimwi

sauti ya kaimu mkurugenzi Rungwe 1

Hata hivyo ametoa wito kwa vingozi mbalimbali kwanzia ngazi ya vitongoji,vijiji,kata na hadi wilaya kutumia mikutano yao kutoa elimu kwenye jamii kuhusu suala la maambukizi ya virusi vya ukimwi

Sauti ya kaimu mkurugenzi Rungwe 2

Dhima kubwa ya mtandao huu ni kuhakikisha unawafikia vijana balehe ukilenga kutoa elimu ya afya ya uzazi na kinga dhidi ya maambukizi ya HIV.

Hatua hii ya kuongezeka kundi kubwa la vijana wanawake limeusukuma mtandao huu kuona namna bora na sahihi ya kulinasua kundi hili muhimu kwa maendeleo ya taifa.

sauti ya mkurugenzi wa mradi

Mradi utawafikia vijana  balehe wanawake wanaoishi katika mazingira hatarishi mathalani wale wanaojiuza katika maeneo mbalimbali na kumbi za starehe .

Mkurugenzi wa Mradi huu Bi. Veronika Lyimo ametaja mikakati ya kuwafikia vijana hawa kuwa ni pamoja kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na mashujaa wawili wanaoishi na Virusi vya Ukimwi huku wakitoa elimu namna ya kujikinga na Maambukizi, matumizi ya dawa za kufubaza virusi, pamoja Ulaji wa chakula lishe kila wakati.

sauti ya mkurugenzi wa mradi kuhusu malengo

Vijana hawa 12 katika vijiji sita watasaidia kuwafikia wanawake wengine zaidi ya 300 katika wilaya ya Rungwe.