Chai FM

Vitendo vya wizi vyaongezeka Rungwe

19 April 2024, 3:16 pm

Wananchi wakiwa kwenye utambuzi wa vitu vilivyoibwa kweye makazi yao

Jamii imeshauriwa kutoa taarifa kwenye viongozi wa maeneo yao bindi wanapo ona vyaashiria ya uwizi au uvunjifu wa amani kwenye maeneo yao.

NA lennox Mwamakula

Wananchi wa mtaa wa Mpindo uliopo kata ya Bulyaga wilayani  Rungwe wamekubaliana kuanzisha ulinzi shirikishi kutokana na vitendo ya wizi vinavyoendelea mtaani hapo.

Mtendaji wa kata ya Bulyaga Heriam Sambo akizungumza na wakazi wa mtaa wa Mpindo kwenye tukio la wizi [picha na Lennox Mwamakula]

Wametoa kauli hiyo ya kuanzisha ulinzi shirikishi kwenye mkutano wa mtaa uliyo itishwa baada ya wakazi wa mtaa huo kuibiwa vitu mbalimbali zikiwemo nguo  na kuvizitelekeza ovyo kwenye  maeneo ya mtaa huo

Baadhi ya vitu vilivyo ibiwa [picha na Lennox Mwamakula]

.sauti za wananchi

Naye mmoja wa watu walio ibiwa na kunusulika kujeruhiwa baada ya kupambana na wezi hao amesema amemtambua mmoja wao kwani alimtolea kisu ili asipige kelele

sauti ya mhanga

Kwa upanda wake balozi wa mtaa huo wa mpindo Ndg Atanas kasebele amezitaja nyumba zilizo kumbwa na adha hiyo ya kuibiwa kwenye mtaa huo kuwa ni takribani nyumba tano na  amesema uongozi umefika kwa kijana aliyekuwa anahisiwa ili kuweza kubaini kama kuna vitu ndani kwake vya wizi

vijana walio hudhuria kwenye mkutano wa mtaa wa mpindo [picha na Lennox Mwamakula]

sauti ya Balozi

Aidha Kasebele  huyo ameitaka  jamii kuwa  na utaratibu wa  kutoa taarifa kwa viongozi wa maeneo yao ili kuweza kuwatabua wageni wanaoingia mtaani hapo

sauti ya balozi ushauri

Sambamba na hilo mmoja wa wajumbe kwenye mkutano huo amesema kinacho pelekea vitendo vya wizi kuendelea mtaani hapo ni watu kuto hudhuria kwenye mikutano pimdi inapo hitishwa na baadhi ya wazazi kuwatetea vijana wao

sauti ya mjumbe

Hata hivyo mtendaji wa kata ya bulyaga Heriam Sambo amesema njia bekee ya kudhibiti vitendo vya wizi ni kuunda ulinzi shirikishi  na kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzie

sauti ya mtendaji