Chai FM

Wanawake wakumbushwa kugombea nafasi za uongozi Rungwe

5 May 2025, 2:50 pm

Katika kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu wanawake wametakiwa ushiriki kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya vyama vyao vya siasa

RUNGWE -MBEYA

Na Bertha Izengo

Wanawake nchini wametakiwa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wakati Taifa tunaelekea kwenye uchagaguzi mkuu October mwaka huu.

Kauli imetolewa na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Rungwe Abdallah Mpokwa alipokuwa kiongea na kituo hiki ofisini kwake amesema nafasi ya kugombea niyakila mmoja hivyo kama chama kinatoa fursa kwa wanachama wote  bila kujali jinsia

Sauti ya katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Bulyaga juu Ndg, Adam Mwaikonyole amesema kwa miaka ya hivi karibuni ushiriki wa wanawake kugombea nafasi mbalimbali kwenye vyama vya siasa unaongezeka siku hadi siku isipokuwa baadhi yao wakuwa nyuma kutokana na kushindwa kujiamini

sauti ya Mwenyekiti wa mtaa

Naye Lwitiko Mbughi  kwa sasa wanawake wamepewa kipao mbele cha kushika nyazifa mbalimbali tofauti na hapo nyuma kutokana usawa ulipo kwenye jamii

sauti ya mwananchi

Aidha Ntuli  Mwansasu  ni moja wa wanawake  ameeleza kuwa hapo awali wanawake hawakupewa nafasi   kutokana mila na desturi zilizopo apo nyuma zilizo kuwa zikimdidimiza mtoto wa kike

sauti za wanawake