Chai FM

Rungwe yakusanya 122.22% ya mapato robo ya kwanza

23 November 2023, 10:18 am

Elimu ya ulipaji wa kodi inayotolewa kwa jamii imeonesha matokeo chanya kwa baadhi ya halmashauri hapa nchini kwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato.

RUNGWE-MBEYA

Na lennox mwamakula

Halmashauri ya wilaya ya Rungwe katika kipindi cha robo ya kwanza kuanzia mwezi Julai mpaka Septemba 2023 imekusanya zaidi ya Shilingi billion 1.888 sawa na Asilimia 122.22 ya Makisio ya shilingi Bill 1.544  kwa kipindi hicho cha robo ya kwanza.

Mapato hayo yaliyokusanywa mwezi Julai mpaka Septemba 2023 ni sawa na asilimia 30.6 ya Makisio ya Mwaka mzima ya Tshs Bill 6.179.

Hayo yamejiri katika baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Rungwe lililoketi mapema leo novemba 22. 2023 katika ukumbi wa John Mwankenja.

Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe[Picha na Lennox mwamakula]

sauti ya makamu mwenyekiti

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe.Jaffar Haniu ameipongeza Halmashauri kwa juhudi za ukusanyaji wa mapato mzuri na kuwa juhudi ziendelee ili Mapato hayo yaendelee kuboresha miundombinu ya kutolea huduma kwa wananchi.

sauti ya mkuu wa wilaya 1

Mhe .Haniu amesema kuwa sehemu kubwa mvua inaendelea kunyesha na wakulima wanalima kwa bidii hivyo ameomba Madiwani kutoa taarifa za upatikanaji wa Mbolea katika maeneo yao ili serikali iweze kuwasambazia Wananchi kwa Wakati.

Aidha amewaomba Wananchi wa Wilaya ya Rungwe kudumisha amani na Utulivu katika maeneo yao hasa katika msimu huu wa Kuelekea sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza[Picha na Lennox mwamakula]
sauti ya mkuu wa wilaya 2

Baadhi ya madiwani halmashauri ya wilaya ya Rangwe wameiomba serikali iweze kutoa mbolea kwa wakati ili kuendana na msimu wa kilimo katika wilaya ya Rungwe.

sauti za madiwani