Chai FM

Wanafunzi waliomajumbani kwa changamoto za ujauzito warudi shule

7 February 2022, 10:58 am

MBEYA

Serikali mkoani Mbeya kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amewataka wanafunzi waliomajumbani kwa changamoto za ujauzito kurudi kuendelea na masomo kwa utaratibu ambao serikali imeupanga.

Homera ameyasema  kuwa serikali ya awamu ya sita kupitia kwa Rais SAMIA SULUHU HASANI  imedhamilia kutoa elimu kwa wote hali itakayotoa fursa kwa wanafunzi waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali kuendelea na masomo.

Ameongeza kuwa kurudi shule kutawasaidi kujiendeleza zaidi na kusaidia kukabiliana na changamoto ya ajira kwani watakuwa na uwezo wa kujiajiri katika kada mbalimbali hata ujasiliamari.

Kwa baadhi ya wanafunzi waliokatisha masomo kwa changamoto  ikiwa ni pamoja na mimba  za utoto  wamemshukuru  Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuruhusu wananfunzi waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali pamoja  na mimba kupewa fursa ya kuendelea na masomo kwa utaratibu maalumu.